Alhamisi 25 Septemba 2025 - 07:22
Damu ya Mashahidi wa Palestina imeamsha dhamira iliyokuwa imelala duniani

Hawza/ Hujjatul-Islam wal-Muslimin Sayyid Sajid Ali Naqvi, Mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa wa Kishia Pakistan, katika hotuba yake akizungumzia hatua ya baadhi ya nchi za Magharibi kuitambua rasmi dola ya Palestina, alisema: Hatua hii ni matunda ya kujitolea kwa taifa la Palestina na ushuhuda wa damu ya mashahidi wake, dhamira ya dunia imeamka, lakini sasa ni wakati wa vitendo.

Kwa mujibu wa Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, Sayyid Sajid Naqvi alibainisha kuwa hatua walizochukua nchi kama Uingereza, Kanada na Australia ya kuitambua Palestina ni matokeo ya damu safi ya mashahidi na matunda ya mwendelezo wa mapambano ya Wapalestina, hususan hukk Ghaza, alisisitiza kuwa damu hizo zimelazimisha hata nguvu kubwa kubadili mitazamo yao.

Akikumbushia nafasi ya kihistoria ya Magharibi katika kuunda na kuimarisha utawala wa Kizayuni, alisema: “Hao ndio waliolipandikiza taifa bandia la Israel katikati ya Mashariki ya Kati na kulisaidia kwa miaka mingi, leo hatua yao huenda ikaonekana chanya, lakini tusisahau kuwa mizizi ya dhulma hii ni mfumo wa kibeberu wenyewe.”

Alifafanua kuwa sasa ni wakati wa serikali kusonga mbele zaidi ya misimamo ya maneno na kuchukua hatua za kivitendo kama vile: kuwaerejesha mabalozi wao nyumbani, kutoa uwekezaji kutoka mabenki yanayohusiana na ukoloni, na kuanzisha vikwazo kamili dhidi ya bidhaa za Marekani na Israel.

Sayyid Sajid Naqvi aliongeza kusema: “Ushindi wa Wapalestina ni kwamba hata zile nchi zilizokuwa ngome ya utawala wa Kizayuni leo zimelazimika kupinga jinai zake na kuitambua Palestina kama dola, hii ni hatua yenye thamani, lakini haitoshi, nchi hizo lazima zikiri hadharani nafasi yao ya kihistoria katika kusaidia uvamizi na pia ziyaombe msamaha mataifa yaliyodhulumiwa.”

Mwisho, alisisitiza kuwa mataifa na serikali zote ambazo kwa miaka zimepaza sauti dhidi ya mauaji ya Wapalestina, leo zinapaswa kuwa na uwajibikaji zaidi: “Kwa kuwa uti wa mgongo wa Uzayuni ni nguvu za kibeberu, na bila kukabiliana nazo kwa dhati, dhulma na jinai zitaendelea.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha